JOKA LA MDIM
UCHAMBUZI WA KAZI YA FASIHI SIMULIZI
JOKA LA MDIM
KIPENGELE CHA FANI.
ZINGATIA:
1. (katika uchambuzi huu mwanafunzi atatakiwa kufahamu muundo na mtindo wa kitabu pamoja na matumizi ya lugha ili kujibu maswali yatayohusiana na kipengele hiki)
2. (matumiz, ya lugha hujumuisha lugha za picha, misemo,nahau na tamathali za semi katika kuwakilisha kazi zao)
3. (kumbuka katika uchambuzi wa vitabu hutumika wakati uliopo(simple present) na hii ni pale unaponukuu baadhi ya maneno katika kitabu)
4.( kuna namna ya kuandika utangulizi(introduction) wakati wa kujibu swali lolote linalohusiana na kitabu cha kuzingatia ni kwamba swali linataka nini ) kwa mfano angalia swali hili "waandishi wengi wa vitabu wamekuwa wakiyaona mambo katika jamii na kuyakosoa ili jamii ibadilike, tumia riwaya mbili ulizosoma kudhihirisha hili"
1. je umefahamu swali linataka nini ? (ujumbe?, maudhui?,au migogoro?)
2.je ni kwa vipi ungeonyesha riwaya utazotumia ?
3. je utaanza na riwaya gani, na utamaliza na ipi ?
4.je utahitimisha vipi insha yako ?
5. je utatumia mifano(quotation) unapotetea hoja zako?
MWANDISHI: ABDALLAH J. SAFARI
MCHAPISHAJI : HUDA PUBLISHERS
MWAKA: 2007
JOKA LA MDIMU image
UTANGULIZI WA KITABU
Joka la mdimu ni riwaya iliyojengwa kwa visa tofautitofauti vinavojengana kukamilisha masimulizi. Ni riwaya inayosawiri au kuakisi mambo yaliyopita ya nyakati za nyuma ambapo kulikuwa na shida kama vile za mafuta ya petroli, Nguo, vyakula nk. Pamoja na hayo zipo pia dhamira au mawazo ambayo yanasawiri maisha ya Mtanzania wa leo kama vile masuala ya rushwa na uhujumu uchumi.
Kwa upande wa fani ni riwaya ambayo mwandishi amewaumba vyema wahusika wake kwa kuwavika uhalisia vyema, amepanga visa vyake na amejitahidi kutumia lugha yenye mvuto na vionjo vya kisanaa huku akiwaburudisha wasomaji kwa mtindo wa kipekee.
JINA LAKITABU
Jina la kitabu limewekwa katika lugha ya picha, JOKA LA MDIMU ni nyoka anayeishi katika miti ya kijani. Nyoka huyu hupendelea kuishi katika miti ya Minyaa na Midimu inayofanana na rangi yake. Nyoka huyu awapo kwenye miti hiyo si rahisi kumtambua kutokana na rangi yake kufanana sana na miti hiyo. Hivyo ni nyoka hatari sana kwa binadamu.
Mwandishi anatumia taswira ya Joka la Mdimu kufananisha na viongozi ambao ni wananchi wenzetu, wanafanana na sisi, ni ndugu zetu damu yetu. Lakini ni hatari mno kwani hutugeuka na kuwa mafisadi, wala rushwa, hawatimizi majukumu yao, ni walaghai nk. Badala ya kusaidia wananchi wao hujali maslahi yao kwanza na hivyo kusababisha mifumo ya kiuchumi kuendelea kuwa migumu kwa wananchi na kupelekea kuongezeka kwa kiasi kikubwa cha watu walio maskini au hohehahe. Hivyo jina la kitabu linasawiri yaliyomo ndani ya kitabu na katika jamii.
FANI
MUUNDO
Riwaya ya Joka la Mdimu imetumia muundo changamani yaani kwa kiasi fulani ametumia rejea au rukia pia ametumia muundo sahili au msago.
Mfano ametumia muundo wa rejea katika sura ya Mindule ambapo anaanza kutueleza juu ya habari za Amani dereva wa taxi na adha anazopata kutokana na ukosefu wa mafuta na jinsi anavyoiendesha biashara yake hiyo. Lakini ndani ya sura hiyohiyo anaturudisha nyuma na kuanza kutuelezea namna Amani alivyopata kazi ya udereva Taxi na kutueleza juu ya mmiliki wa Taxi hiyo ambaye ni Shiraz Bhanj. Pia katika sura ya Boko anatueleza juu ya Safari ya Tino kwenda kumuona mwanae mgonjwa uk.73 ila hatuelezi inavyoendelea lakini anarukia kisa kingine cha Brown Kwacha na sura ya Kwale halafu badae anaturudisha nyuma na kuendelea kutuelezea juu ya habari za kuuguliwa kwa Cheche na Tino anapofika kumuona katika sura ya Dakta Makwati. Pia ametumia muundo wa moja kwa moja katika sura zingine kwani ameyapanga matukio yake katika usahili bila kuruka.
Pia mwandishi amegawanya visa na mtukio katika sura kumi ambapo kila sura ameipa jina kwa kutumia majina ya wahusika.
Sura ya kwanza, MINDULE
Hapa mwandishi anatueleza kuhusu habari za Amani dereva Taxi, masaibu anayopata katika kazi yake kutokana na uhaba wa mafuta katika vituo vya mafuta.
Sura ya pili, TINO
Hapa tunaelezwa kuhusu maisha ya Tino na kazi anazofanya ya kuvuta kwama. Tunaambiwa kuhusu hali ngumu ya maisha ya Tino na wakazi wengine wa Sega, hapa tunaelezwa pia kuhusu masuala ya uongozi jinsi ulivyo mbovu na ugawanywaji mbovu wa vyanzo vya uchumi na bidhaa.
Sura ya tatu, JINJA MALONI
Katika sura hii tunaelezwa kuhusu maisha ya Jinja Maloni, hapa anaibua dhamira kama vile za uvamizi, uhalifu na mauaji pia anaendela kutueleza kuhusu hali ngumu ya maisha.
Sura ya nne SEGA
Maisha ya wakazi wa Sega yanaelezewa hapa jinsi yalivyo ya dhiki, pia tunaelezwa kuhusu Tino na mkewe maisha yao yalivyo na familia yao, anaibua dhamira ya mapenzi ya dhati na upendo kwa familia.
Sura ya tano, BOKO
Hapa tunaelezwa kuhusu adha ya usafiri kwa watu, shida ya mafuta, ubovu wa miuondmbinu kama vile barabara, vinasemwa hapa.
Sura ya sita, BROWN KWACHA
Sura hii inaeleza habari za Brown maisha yake na tabia zake, anaibua dhamira kama vile uhujumu uchumi, biashara za magendo, suala la kutowajibika kwa watumishi, suala la kukosekana kwa uaminifu katika ndoa na mapenzi ya pesa ambapo sifa zote hizi alizibeba Kwacha.
Sura ya saba, KWALE
Hapa yanaelezwa mambo kuhusu hifadhi ya Kwale, safari ya Brown na Leila kwenda kutembea kwale. Hapa yanatajwa mambo ya udhalimu wa kuharibu mali za umma (maliasili za taifa) mfano pembe za ndovu, vipusa pia mapenzi yasiyo ya kweli.
Sura ya nane, DAKTA MIKWALA
Dakta Mikwala ndiye mhusika mkuu anayeelezwa hapa, tunalezwa juu ya ugumu wa upatikanaji wa huduma za afya kwani Cheche anashindwa kutibiwa kutokana na ukosefu wa fedha za kigeni.
Sura ya tisa, CHECHE
Tunaelezwa juu ya juhudi za Amani na Tino ili kumsaidia Cheche aweze kwenda kutibiwa Uingereza. Wanafanikiwa kupora benki na kupata pesa za kumtibu Cheche.
Sura ya kumi, MOTO
Hapa hatma ya visa vidogo vidogo imeelezwa kwa kutolewa hatma ya maisha ya Cheche na Brown Kwacha. Cheche alipata matibabu na kupona na Browna anafanikiwa kuirubuni serikali kwa kuipanga mahesabu ya uongo.
MTINDO
Mwandishi ametumia mitindo ya aina tofautitofauti ili kuweza kuipamba kazi yake ivutie.
Matumizi ya nafsi.
Matumizi ya nafsi ya tatu Umoja. Imetawala.
Mfano uk.5 Amani aliangalia. Uk.25 Amani alijizuia .
Nafsi ya tatuwingi; mfano uk. 63 wote walitoka nje kuelekea klabuni.
Pia uk.53 wale wanaume walimvamia
Matumizi ya nafsi ya pili.
Mfano uk.106 mmechoka kuangalia video? aa tumeshaziona mara nyingi tunaomba aina nyingine . Mazungumzo baina ya mke wa Brown na wanae.
Pia mazungumzo baina ya Brown na Leila.
Uk.113. habari za asubuhi
Nzuri sijui wewe alijibu
Uliota njozi njema?
"Wapi?"
"Kwa nini?"
Matumizi ya nafsi ya kwanza.
Mfano uk. 39 mimi nimemaliza .kuiba nimeiba sana.
Matumizi ya nyimbo. Uk . 70 . wimbo wa Chaupele
Chaupele mpenzi, haya usemayo
Kama ni maradhi, yapeleke kwa Daktari
Wanambia niache rumba, na mimi sikuzoea
Sitaweza kuliacha rumba, kwa sababu yako
Kama wanipenda, nenda kwa baba
Pia uk.58 sega! Sega! Sega!, usioogope wimbo waliouimba washabiki wa michezo.
Masimulizi ya hadithi ndani ya hadithi.
Hapa mwandishi amemtumia muhusika kusimulia kisa kingine kidogo ndani ya kisa kikuu. Mfano uk . 39 mhusika Tino anamsimulia mteja wake maisha yake ya mwanzo kabla hajaanza kazi ya kuvuta kwama.
MATUMIZI YA LUGHA
Mwandishi A. Safari ametumia lugha fasaha na inayoeleweka kwa wasomaji wake. Kuna matumizi ya lugha nyinginezo kama vile kiingereza. Uk.55 city devils uk.155 I miss my family, uk.24 Hey man you will pay extra money, uk.99 consignment. Pia kuna matumizi ya lugha ya kiarabu, mfano uk.45 Salaam aleikum mayitun uk.42 Inna Ilayhi Raajiunna!, uk.13, Insha Allah! . Vilevile kuna matumizi ya lugha ya mtaani uk.39 msela, ndito, kashkash.
Matumizi ya tamathali za semi.
Tashibiha
Uk.117 ngozi yake nyeusi kama udongo wa mfinyanzi
Uk.122 mweusi kama sizi la chungu
Uk.9 Zepher 6 ile iliunguruma kama simba dume
Uk.10 mteuzi mithili ya Mbega
Uk.35 miguu yake ikakazana mithili ya upinde uliotaka kufyatuliwa
Sitiari
Uk.91 Brown Kwacha alikuwa kinyonga
Uk.15 sarahange wetu mboga kweli siku hizi
Uk.40 huku twakaa vinyama vya mwitu
Uk.72 sote ni kobe
Tashihisi
Uk.109 gari lile zuri lilioondoka kwa madaha
Uk.143 kuta nyeusi za nyumba zaidi ya kumi zilisimama twe!kuomboleza
Uk.91 pua zake zikalakiwa na riha na ashrafu ya manukato
Uk.12 utumbo ulimlaumu
Uk.27 mvua ikapiga kwa kiburi na kuviadhibu vibati vibovu.
Tafsida
Uk. 49 isijekuwa nimekukatiza haja!, pia uk. hohuo kinyesi.
Mbinu nyingine za kisanaa.
Takriri
Uk.151 mwizi! Mwizi! Jambazi! Jambazi!
Uk.57 shinda! Shinda! Shinda!
Uk.33 karibu baba, kariibu kaka, karibu mkwe
Uk.72 uhuru upi? Uhuru gani? Uhuru wa nini na nani?
Mdokezo
Uk.149 lakini..
Onomatopea au tanakali sauti
Uk. 1 saa mezani niliendelea kugonga taratibu ta! ta! ta!
Uk.10 ikatoka sauti kali tupu ta nye nye
Uk.67 upepo wa stova uliolia shshsh
Tashtiti
Uk.113 . leila anamuuliza Brown maswali ambayo anayajua majibu yake.
Brown: uliota njozi njema?
Leila : Wapi?
Leila: Kwanini?
Brown: Mwenywe unajua
Nidaa
Uk.39 Aaa! Limbukeni wa jiji anataka kunitia kashkash
Uk 30 nguo zangu Mungu wee!
Uk.42 Inna Lillah wa Inna Ilayhi Raajiunna!
Uk.92 Ah! Leila kwacha alimsalimia kwa furaha
Uk. 105 Lahaula
Matumizi ya Semi.
Methali
Uk.78 asilojua mtu ni usiku wa kiza
Uk.83 ukiona mwenzako anyolewa zako tia maji
Uk.98 mtaka waridi sharti avumilie miiba
Uk. 99 biashara haigombi
Uk.43 ajizi nuksani huzaa mwana kisirani
Misemo
Uk.10 asiye na bahati habahatishi
Uk.47. asiyezika hazikwi
Uk.64 mmetupa Jongoo na mtiwe
Uk.98 asali haichomvwi umoja
Uk.111 ajali haina kinga
Uk.115 mwenye macho haambiwi tazama
Uk.120 matendo hushinda maneno
Uk.47. asiyezika hazikwi
Nahau
Uk.11 sio unanilalia kila mara kunidhulumu
Uk.107 alikonda akajipa moyo kujifariji moyo
Matumizi ya taswira
Taswira mwonekano imetumika, ambayo inatujengea picha kutokana na vitu tunavyovifahamu. Mfanouk.76 alisema kijana mmoja wa kiume kavaa sketi, blauzi na sidiria iliyopachikwa juu yake. Kichwani alifunga kilemba. Hii inatupa picha halisi ya huyo kaka kwani tunaposoma ni kama kweli tunamuona kutokana na jinsi mwandishi alivyoelezea. Pia uk.135 mwambie yule jamaa pale atayarishe kuku mzuri wa kukaanga na kachumbari yenye pilipili hii inamfanya msomaji ahisi ladha ya kuku na hiyo pilipili kwa maneno ambayo mwandishi ameyajengea taswira na hii ni taswira hisi.
la mdimu ni taswira ya nyoka mbaya ambaye amefananishwa na viongozi wabaya.
WAHUSIKA
AMANI
Ni dereva taxi
Ana upendo wa dhati
Ni mchapakazi
Ana hekima na busara
Ana huruma
Ni rafiki wa kweli wa Tino
Kutokana na hizo sifa amani ni mhusika bapa
Anafaa kuigwa na jamii
TINO ( mhusika bapa )
Ni mchapakzi
Mlezi bora wa familia
Baba wa Cheche
Ana huruma
Ana upendo wa dhati
Ni makini
Ni jasiri
Ni mwanamichezo
Anafaa kuigwa na jamii
BROWN KWACHA
Ni mkurugenzi wa idara ya fedha za kigeni
Ni muhuni na Malaya
Fisadi na mla rushwa
Anafanya biashara haramu
Hana mapenzi kwa familia yake
Anapenda anasa
Si muaminifu kwa mkewe
Si muadilifu
Hafai kuigwa na jamii
Ni mhusika bapa
JINJA MALONI
Ni jasiri na mwenye nguvu
Ana huruma na upendo
Mchapakzi
Mlevi
Maskini
Ni mhusika duara
DAKTARI MIKWALA
Ni daktari bingwa wa mifupa
Anapenda rushwa
Si muwajibikaji katika kazi yake
Ni mlevi
Hafai kuigwa na jamii
Ni mhusika bapa
SHIRAZ BHANJ
Ni mfanyabiashara
Ni mtoa rushwa
Ana biashara za magendo
Rafiki wa Brown
Hafai kuigwa na jamii
Ni mhusika bapa
ZITTO
Ni mfanyakazi bandarini
Ni mwanamichezo
Ni jasiri ana kipato duni
Rafiki wa Tino na Amani
CHECHE
Ni mtoto wa Tino
Ana nidhamu na bidii
Ni mwanamichezo
Ana upendo kwa wazazi wake
Ni mtiifu na msikivu
Mcheshi na mudadisi
Alivunjika kiuno michezoni
Ni mhusika bapa
MWEMA
Ni mke wa Tino
Mvumilivu
Ana mapendo ya dhati kwa familia yake
Ni mchapakazi
Ni mhusika bapa
JOSEPHINE NA LEILA
Wasichana wahuni waliojiuza kwa Brown Kwacha
Hawafai kuigwa na jamii
MANDHARI
Mandhari aliyoitumia mwandishi ni ya mjini, anataja baadhi ya maeneo ya nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kama vile Boko, Sega, Mindule. Mandhari hii ni sadifu kwa yale ambayo mwandishi ameyaeleza kwani masuala ya rushwa, upotevu wa haki, hali ngumu ya uchumi na maisha kwa ujumla, ni matatizo halisi ya jamii ya Tanzania
Saturday, February 8, 2020
TAMTHILIYA; KILIO CHETU
MWANDISHI; MEDICAL AID FOUNDATION
MCHAPISHAJI; TANZANIA PUBLISHING HOUSE
MWAKA; 1995
Kilio chetu ni tamthiliya inayovunja ukimya uliotawala miongoni mwa jamii katika kutatua matatizo makubwa ambayo chimbuko lake ni mahusiano ya kijinsia.
Katika tamthiliya hii vijana wanatoa sauti ya jitimai iliyojaa sononeko na shutuma dhidi ya wazazi, walezi na viongozi ambao wanafumbia macho suala hili nyeti. Ndiyo maana tamthiliya hii inasisitiza sana haja ya kuwapa vijana elimu juu ya mahusiano ya kijinsia badala ya hofu na vitisho ambavyo vimedhihirika kupitia hali halisi ya kuwa vimeshindwa.
FANI
MUUNDO
Tamthiliya hii imetumia muundo wa moja kwa moja. Inaanza kwa kutuonesha wazazi wakibishana juu ya kutoa elimu ya jinsia na mahusiano. Mwisho Joti mtoto ambaye hakupatiwa elimu hiyo anampa mimba mtoto mwenzake Suzi. Baadae Joti anakufa kwa UKIMWI.
Pia tamthiliya hii imegawanywa katika sehemu sita.
sehemu ya kwanza. Inaonesha jinsi ambavyo gonjwa la UKIMWI linaiteketeza, jamii wengi wao wakiwa watoto ambao hawakuwa na elimu ya jinsia na mahusiano.
sehemu ya pili. Wazazi wanabishana juu ya kuwapatia elimu ya jinsia na mahusiano watoto wao. Mama Suzi anasema jambo hilo liko kinyume na maadili, lakini Baba Anna yeye anaunga mkono suala hilo.
sehemu ya tatu. Inaeleza kuhusu watoto Joti na Suzi ambao wamekwisha anza mambo ya ngono. Pia watoto wameathiriwa na utandawazi kwani wanaangalia video za ngono bila wasiwasi.
Sehemu ya nne. Inazungumzia tabia hatarishi za Joti kuwa na wasichana wengi. Vilevile Anna kutokana na elimu ya jinsia na mahusiano aliyonayo, anaendelea kukwepa vishawishi.
Sehemu ya tano. Mtoto Suzi kapata mimba, anabaki njia panda akiwa hajui afanye nini.
Sehemu ya sita. Hii ni sehemu ya sita. Tunamuona Joti akifa kwa UKIMWI, na Suzi anabaki akiwa na mimba pamoja na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
MTINDO
Tamthiliya hii imetumia mtindo wa;
i. Dayolojia majibizano ya wahusika yametawala toka mwanzo mpaka mwisho wa tamthiliya hii.
ii. Monolojia mtindo huu wa masimulizi umetumika japo kwa kiasi kidogo.
iii. Mtindo wa masimulizi ya ki ngano - mfano katika ukurasa wa 1 Mtambaji anasimulia,
Hapo zamani za kale paliondokea kisiwa kimoja kikubwa sana. Kisiwa kilikuwa na watu wa kila aina
iv. Matumizi ya nyimbo katika ukurasa wa 29, Anna anaimba wimbo unaokemea wanaume wanaomfuata kumlaghai.
Anna, Anna, Anna mie niacheni mie x 2
Msichana mdogo bado ninasoma niacheni mie.
v. Matumizi ya nafsi
Nafsi zote zimetumika lakini nafsi ya pili imetawala zaidi.
WAHUSIKA
JOTI
Mhusika mkuu
Hana elimu ya jinsia na mahusiano
Anajiingiza katika mahusiano ya kimapenzi na wasichana wengi. Wengine wakiwa wakubwa kuliko yeye.
Mwisho anakufa kwa UKIMWI
SUZI
Mhusika mkuu
Msichana mdogo anayesoma shule ya msingi
Hana elimu ya jinsia na mahusiano
Anajiingiza katika mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi mwenzake Joti, pia anaambukizwa UKIMWI na kupata mimba.
ANNA
Msichana mwenye elimu ya jinsia na mahusiano
Anakataa vishawishi vya wanaume kwa sababu anajitambua kwa sababu ya kuwa na elimu ya jinsia
MAMA SUZI
Anashikilia mila na tamaduni za zamani
Haungi mkono kuwapatia watoto elimu ya jinsia na mahusiano, anaamini kufanya hivyo ni kuwaharibu watoto
MJOMBA
Mwanaume mtu mzima
Anaunga mkono wazazi kuwapatia watoto wao elimu ya jinsia na mahusiano.
Wahusika wengine ni; Baba joti, Mama Joti, Baba Anna, Choggo, Mwarami, Jumbe, Chausiku, Jirani, na wengineo.
MANDHARI
Mandhari ya mjini yametumiwa na mwandishi. Pia kunayo mandhari ya;
Nyumbani, kijiweni, barabarani, n.k
MATUMIZI YA LUGHA
Tamathali za semi
i. Tashibiha. Wakapukutika kama majani ya kiangazi. Uk 1
ii. Sitiari. We mbwa mweusi. Uk 10
iii. Takriri . vikawazoa, vikawazoa vikawazoa. Uk 3
iv. Tanakali sauti. pwi, pwi, pwi, uk 18
v. Tafsida. Kafa kwa kukanyaga nyaya. Uk 4
vi. Mubaalagha. mtu si mtu, kizuka si kizuka uk 4
Misemo, nahau na methali
i. Msemo. Wembamba wa reli treni inapita. Uk 7
ii. Msemo. Kukimbilia suti na nepi hujavaa. Uk 28
iii. Methali. umeula wa chuya. Uk 29
iv. Methali. shukrani ya Punda ni mateke uk 19
v. Nahau. nimekuvulia kofia uk 6
Picha na taswira
Dubwana ugonjwa wa UKIMWI;
Nguru aina ya Samaki wabayaamefananishwa na mtu mbaya;
Kinyago - Suzi.
MAUDHUI
DHAMIRA
Dhamira nyingi zimejadiliwa katika tamthiliya hii, miongoni mwa dhamira hizo ni;
i. Elimu ya jinsia na mahusiano.
Jamii imekumbwa na mmomonyoko mkubwa wa maadili pamoja na maradhi hatari yasiyotibika kama UKIMWI. Hivyo wazazi wanapaswa kuwaelimisha watoto wao juu ya njia sahihi za kujikinga na matatizo haya. Katika tamthiliya tunaona pande mbili, ule unaoshikilia ukale na upande unaotaka mabadiliko. Baba Anna, anawaelimisha watoto wake juu ya madhara ya kujihusisha na ngono katika umri mdogo, Anna anaelewa na anafanikiwa kukwepa vishawishi. Hali ni tofauti kwa Mama Suzi anaamini kuwapatia watoto elimu ya jinsia na mahusiano ni kuwaharibu na kuwapoteza. Anaposhauriwa kuwapatia watoto elimu hiyo anafoka,
Huko si ndiko kunifundishia wanangu umalaya? Umfunze mwanangu habari za ngono
Kutokana na kutokukubali kuwapatia wanawe elimu hii, Suzi anapewa mimba na kuambukizwa UKIMWI.
ii. Mmomonyoko wa maadili.
Maadili hayazingatiwi tena katika jamii. Watoto kwa wakubwa wote wamepotoka. Tunaona watu wazima wakitembea na watoto wadogo, mfano Chausiku anamahusiano na mtoto mdogo Joti. Pia watoto wamejiingiza katika mahusiano ya kimapenzi, Joti anamahusiano na Suzi. Watoto hawahawa wanaangalia video za ngono bila kuogopa chochote. Katika ukurasa wa 20 Joti anasikika akiwahamasisha wenzake.
Yaap, ukimtaka Suzi, chukua. Picha ya ngono, matusi angalia!
Mmomonyoko huu wa maadili utaondolewa endapo watoto watapatiwa elimu.
iii. Athari ya sayansi na teknolojia. Maendeleo ya sayansi na teknolojia yameleta mabadiliko makubwa katika jamii, mfano katika tamthiliya hii, watoto wanakwenda kuangalia picha za ngono na kuwafanya waharibikiwe kifikra kwa kutamani kuigiza kile wanachokiona. Joti, mtoto kinara wa kutazama picha hizo anaambulia UKIMWI na kufa angali mtoto mdogo.
iv. Nafasi ya mwanamke katika jamii. Nafasi ya mwanamke ni jumla ya mambo yote ayatendayo mwanamke katika kazi ya fasihi. Mengine huwa mazuri yanayostahili pongezi na machache huwa mabaya yanayostahili kukemewa kwa nguvu. Katika tamthiliya hii, mwanamke amechorwa kama;
Chombo cha starehe. Mfano Joti anamtumia Suzi kwa ajili ya kujistarehesha.
Asiyependa mabadiliko. Mama Suzi hataki kutoa elimu ya jinsia kwa wanaye.
Asiye na maadili. Suzi hana maadili, anajiingiza katika mahusiano ya kimapenzi katika umri mdogo.
Mwenye elimu na asiyedanganyika. Anna ana elimu ya jinsia na mahusiano, wanaume wanashindwa kumdanganya kwa pesa na maneno matamu.
UJUMBE
i. Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu. Suzi na Joti hawakufunzwa vyema na wazazi wao, badala yake ulimwengu unawafunza.
ii. Elimu ya jinsia na mahusiano itolewe kwa watoto. Elimu hii itawafanya waepuke vishawishi.
iii. Sheria kali zitungwe dhidi ya watu wanaowalaghai watoto. Kuna watu wazima wanaowaingiza watoto katika vitendo vya kimapenzi kama Chausiku anavyomlaghai Joti. Sheria kali itungwe na isimamiwe kuwakomesha.
iv. Wazazi wote washirikiane katika malezi ya watoto. Baba Anna na Mama Anna wanashirikiana katika malezi ya watoto wao. Matokeo bora yanaonekana.
MIGOGORO
Migogoro iliyojitokeza ni pamoja na;
Migogoro ya wahusika
i. Mgogoro wa Joti na Suzi.
Mgogoro huu unasababishwa na tabia ya joti kuwa na mahusiano na wasichana wengi. Suluhisho la mgogoro huu ni Joti kumuomba msamaha Suzi.
ii. Mgogoro wa Suzi na Mama yake.
Mgogoro huu unasababishwa na mama Suzi kuvikuta vidonge vya kuzuia mimba katika sketi ya mwanaye. Suluhisho la mgogoro huu ni Mjomba kumwamuru Suzi aende ndani na mazungumzo kati ya Mjomba, Mama Suzi na majirani wengine yanaendelea.
iii. Mgogoro kati ya Mjomba na Mama Suzi.
Chanzo cha mgogoro huu ni Mjomba kumshauri Mama Suzi ampe elimu ya jinsia na mahusiano binti yake. Mama Suzi anakataa na kusema kufanya hivyo ni kuwafundisha watoto umalaya.
iv. Mgogoro kati ya Chausiku na Joti.
Chausiku anamlaumu Joti kuwa anamahusiano na wasichana wengine, anaendelea kulalama kuwa, hata zawadi anazompatia anawapatia wasichana wengine. Chausiku anamtisha Joti kuwa atamchoma moto yeye na visichana vyake. KICHEKO!!
Mgogoro wa nafsi
Huu ni mgogoro ambao humpata mhusika peke yake kati yake yeye na nafsi yake.
Suzi anapatwa na mgogoro wa nafsi pale anapopata mimba na kuambukizwa virusi vya UKIMWI. Anabaki akilia, lakini hakujilaumu mwenyewe, bali anamlaumu mama yake kwa kushindwa kumpatia elimu ya jinsia na mahusiano. Katika ukurasa wa 40, anasema,
Mimi na Joti tungepata bahati ya kuelimishwa tusingetumbu
MSIMAMO
Mwandishi anamsimamo wa kimapinduzi. Katika tatizo la watoto wengi kuangamia kwa ugonjwa wa UKIMWI, anashauri elimu ya jinsia na mahusiano itolewe ili kuleta ukombozi kwa jamii.
FALSAFA
Mwandishi anaamini kuwa elimu ya jinsia na mahusiano ikitolewa kwa watoto itawasaidia kupambana na hatari ya kuambukizwa virusi vya UKIMWI.
KUFAULU NA KUTOKUFAULU KWA MWANDISHI
KUFAULU
Kufaulu katika fani
Mwandishi ametumia lugha nyepesi inayoeleweka kwa urahisi.
Mwandishi ametumia wahusika ambao wameibeba vizuri dhamira kuu
Mwandishi ametumia muundo rahisi wa moja kwa moja ambao haumchoshi msomaji wal a kumchanganya.
Kufaulu kwa maudhui
Mwandishi amefaulu kufikisha dhamira katika jamii juu ya umuhimu wa kuwapatia watoto elimu ya jinsia na mahusiano.
Pia mwandishi ameifungua jamii na kuionya juu ya hatari ya sayansi na teknolojia endapo itatumiwa vibaya.
KUTOKUFAULU
Kutokufaulu katika fani
Mwandishi ametumia mandhari ya mjini pekee kana kwamba maambukizi ya virusi vya UKIMWI yanawakabili watoto waishio mjini tu.
Kutokufaulu katika maudhui
Ugonjwa wa UKIMWI huwapata watu wote bila kuzingatia umri. Lakini katika tamthiliya hii, wanaougua ugonjwa huu ni watoto pekee. Kwa kiasi fulani mwandishi hajafaulu.
Hata hivyo kazi hii ni bora na inastahili pongezi kwa mafunzo makubwa inayoyatoa katika jamii yetu iliyogubikwa na utandawazi.

Jina la kitabu: ORODHA
Mwandishi: Steve Reynolds
Mwaka: 2006
Tamthiliya hii ya Orodha inahusu suala zima la UKIMWI na athari zake katika jamii. Mhusika mkuu Furaha na wahusika wengine, wametumiwa kuonesha athari za gonjwa hili lakini pia mbinu za kupamban na UKIMWI, zimechorwa vyema.
JINA LA KITABU
Jina hili (ORODHA) linasadifu yaliyomo. Mhusika Furaha anaandika orodha ya kusomwa kwa sauti wakati wa mazishi yake ambayo jamii ya kijiji inaamini inafichua majina ya watu waliomwambukiza virusi vya UKIMWI. Orodha inayotolewa na mhusika furaha ambayo aliomba isomwe katika mazishi yake ni, uwazi, ukweli, uadilifu, uelewa, upendo, elimu, uwajibikaji na msamaha.
MAUDHUI
Maudhui ni jumla ya mawazo yote yanayozungumzwa katika kazi za fasihi, pamoja na mtazamo wa mwandishi juu ya mawazo hayo.
Vipengele vya maudhui ni pamoja na , dhamira, migogoro, falsafa, ujumbe na msimamo.
DHAMIRA
i. Athari na mapambano dhidi ya gonjwa la
UKIMWI . Mwandishi anamtumia mhusika Furaha kuonesha athari ya gojwa hili, lakini pia, mapambano makali dhidi yake.
Furaha anakufa akiwa katika umri mdogo, lakini anaacha orodha ambayo itaongoza mapambano dhidi ya UKIMWI.
Katika miezi ya mwisho, nimelala kitandani, nikifa, nikizidi kuugua.. katika ukurasa unaofuata kuna orodha ya vitu ambavyo vilisaidia kuyafupisha maisha yangu. (Uk 44)
Mapambano ya UKIMWI, yataongozwa kwa kuzingatia mambo haya, uepukaji, matumizi ya kondomu, uaminifu, elimu, uelewa, uwazi, uadilifu, uwajibikaji, ukweli, upendo na msamaha.
Dhamira zingine zinazojitokeza katika tamthiliya ya Orodha ni pamoja na:
ii. Mmomonyoko wa maadili. Mhusika furaha hana maadili, anatoroka nyumbani usiku wa manane na kwenda baa kunywa pombe na wanaume. Furaha anasikika akisema,
Sawa, lakini nakunywa kidogo tu hapa (uk 8)
Vilevile, mtumishi wa Mungu, padri James ambaye ndiye alitakiwa ahakikishe maadili yanakuwepo katika jamii yake, anamlaghai furaha na ufanya naye mapenzi. Padri James anasikika akisema,
Mlango utakuwa wazi taa zitakuwa zimezimwa kuficha utambulisho wako. Usimwambie mtu yeyote mwanangu. Njoo peke yako
iii. Athari za marafiki. Furaha anapotea kwa sababu ya ushauri mbaya anaopewa na rafiki yake Mary. Mary ndiye anayemfundisha Furaha kutafuta wanaume na kunywa pombe. Katika ukurasa wa tano, Mary anasikia akimnongoneza Furaha, Furaha Psss Furaha! Haraka wanatusubiri kule baa!
iv. Suala la mapenzi. Suala hili limejadiliwa katika nyanja mbili. Mapenzi ya kweli na mapenzi yasiyo ya kweli. Kwa upande wa mapenzi ya kweli, tunawaona baba na mama Furaha wakimuonya mtoto wao dhidi ya tabia yake mbaya. Hawa wanampenda binti yao, hivyo hawataki kumuona akipotea. Kwa sauti ya upole kiasi, mama Furaha anasikika akisema, Hivi sasa umemaliza shule. Lazima uyafikirie maisha yako ya siku za baadaye. (uk 21).
Upande wa mapenzi yasiyo ya kweli, wahusika Bwana Ecko, Bwana Juma, Kitunda, Mary, Padri James na Salim, hawana mapenzi ya kweli kwa furaha, wao walitaka kumtumia kwa starehe zao.
v. Hofu. Jamii inagubikwa na hofu kuu juu ya ugonjwa wa UKIMWI. Wanakijiji katia kijiji cha Furaha hawajui chanzo hasa cha gonjwa hilo. Wengine wanadhani inatokana na uchawi, wengine wakidhani pengine kwa sababu ya kugusana. Pamoja na kuliogopa gonjwa hilo, wanakijiji hawa hawaonekani kuzijua njia za kujikinga na maradhi haya.
Hofu inatanda kwa Salim, Padri James, Bw. Ecko na Kitunda pale wanaposikia kuwa Furaha kaacha Orodha. Wote hawa wanahangaika kuitafuta Orodha iliyoachwa bila mafanikio. Bwana Ecko anapomuona Kitunda ameingia katika chumba ilimolazwa maiti ya Furaha, anachimba mkwara kwa Kitunda. Ni wewe Kitunda, unafanya nini hapa, mtoto wewe? Unawezaje kuthubutu, nitakufanya ukamatwe!
vi. Nafasi ya mwanamke katika jamii. Hii ni jumla ya mambo yote ambayo yanafanywa na mwanamke katika jamii yake. Wakati mwingine mwanamke hufanya mambo mema yenye kufurahisha, lakini pia mwanamke huweza kufanya mambo mabaya yenye kukera. Katika Tamthiliya hii, mwanamke amechorwa katika nyanja zifuatazo:
a. Chombo cha starehe. Wanaume wanaonekana kumtumia mwanamke kama chombo cha starehe. Furaha anatumiwa na akina Bwana Ecko na wenzake kwa lengo la kuwaburudisha.
b. Pia, mwanamke amechorwa kama jasiri anayesema ukweli. Furaha ni mwanamke jasiri, anaandika orodha ya mambo yote ambayo yamemfanya aambukizwe UKIMWI.
c. Mama mlezi wa familia. Mama Furaha anajitahidi sana kuilea familia yake. Hasiti kumshauri Furaha pale anapokosea.
d. Asiye na maadili. Msichana Marry na Furaha hawana maadili yanayotakiwa katika jamii. Wanawake hawa wanakunywa pombe na wanaume usiku wa manane.
UJUMBE
Haya ni mafunzo mbalimbali ambayo hupatikana baada ya kusoma kazi ya fasihi. Mafunzo yanayopatikana katika tamthiliya hii ni:
i. Elimu kuhusu UKIMWI. Itolewe kwa wanajamii. Wanajamii wanapaswa kuelimishwa zaidi ili wajue nini maana ya UKIMWI na mbinu za kuepukana na maradhi haya. Katika kitabu, mwanakijiji 1, hana elimu yoyote kuhusu UKIMWI, kama asemavyo:
Rahisi! Kuna mtu kamroga Pengine rafiki msichana mwenye wivu.
Mwanakijiji huyu anaamini kuwa maradhi haya huenezwa kwa njia ya uchawi.
ii. Uepukaji, matumizi ya Kondomu, uaminifu, elimu, uelewa, uwazi, uadilifu, uwajibikaji, ukweli, upendo na msamaha vitayafuta na kuyaondoa kabisa maradhi ya UKIMWI
iii. Ugonjwa wa UKIMWI upo na unaua. Ugonjwa huu unaua! Mhusika Furaha anapoteza maisha na kuiacha familia yake ikiwa na hudhuni. Mwandishi anakumbusha wanajamii kuchukua tahadhari.
iv. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Furaha anashindwa kusikiliza ushauri wa wazazi wake. Anaamini kufuata mienendo yake mibaya mwisho anakufa kwa UKIMWI.
MIGOGORO
Ni mvutano, misuguano na kukosekana kwa maelewano katika ngazi ya fasihi. Migogoro inaweza kuwa kati ya wahusika, ama inaweza kuwa ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na migogoro aya nafsi.
Migogoro ya wahusika
i. Baba Furaha na Furaha. Mgogoro huu unasababishwa na Furaha kuanza mienendo mibaya. Suluhisho la mgogoro huu ni Furaha kumkanya binti yake huyo asiendelee na tabia yake mbaya isiyoridhisha.
ii. Salim na Furaha. Huu unasababishwa na Furaha kumnyima orodha kijana Salim. Suluhisho la mgogoro huu ni Salim kuamua kuondoka na kumuacha Furaha akikata roho.
iii. Dada mdogo na Furaha. Huu unasababishwa na Dada Mdogo kumuona Furaha akijaribu kutoroka kupitia sehemu ya dirisha. Suluhisho la mgogoro huu ni Furaha kutishia kumchinja Dada Mdogo.
Mgogoro wa nafsi
Mgogoro huu unampata Furaha. Anapata majuto makuu kuhusiana na mambo yote aliyoyatenda hadi kupekelekea kuambukizwa virusi vya UKIMWI. Suluhisho la mgogoro huu ni Furaha kuandika Orodha ambayo itatoa funzo kwa wanajamii ili waweze kuepuka mambo yote yasababishayo UKIMWI.
Migogoro ya kiuchumi
Uchumi mdogo (umasikini) alionao Furaha, ndio unaomfanya apate tamaa ya kujiingiza katika mahusiano na wanaume wenye pesa kama akina Bwana Ecko, ambaye ni tajiri mkubwa kijijini pale. Mzee huyu alimilika baa, aliwatapeli wasichana wadogo kwa fedha zake na vijizawadi vidogovidogo.
Falsafa
Hii ni imani ya mwandishi katika kazi yake ya fasihi. Katika tamthiliya hii, mwandishi Steve Reynolds anaamini kuwa, kutoa elimu ya kutosha kuhusu ugonjwa wa UKIMWI kutapunguza maambukizi.
Msimamo
Ni ile hali ya mwandishi kuamua kufuata na kushikilia jambo fulani. Mwandishi wa tamthiiya hii ana msimamo wa kimapinduzi, kwani anajadili mambo yanayosababisha kutokea kwa ugonjwa wa UKIMWI. Pia anaonesha suluhisho la matatizo hayo, anatilia mkazo suala la kutolewa elimu.
Fani
Ni ufundi wa kisanaa autumiao msanii katika kufikisha maudhui aliyokusudia. Fani imegawanyika kataka vipengele vitano ambavyo ni: wahusika, muundo, mandhari, matumizi ya lugha na mtindo.
MUUNDO
Mwandishi ametumia muundo rejeshi. Katika sehemu ya kwanza na ya pili, anatuonesha mahali yanapofanyika mazishi ya Furaha. Sehemu ya tatu na 20 anatuonesha juu ya maisha ya Furaha mpaka kifo chake.
Mwandishi ameweka kazi yake katika onyesho moja. Katika onyesho hilo ameweka sehemu ndogondogo 20 zinazojenga na kukamilisha tamthiliya nzima.
MTINDO
- mtindo wa dayolojia au majibizano. Mfano:
Baba: unafanya nini binti yangu?
Furaha: Sifanyi kitu baba
- Mtindo wa monolojia au masimulizi. Mfano: sehemu ya baa. Furaha na Mary wanatazamana kutokea pembeni wakati Bwana Ecko akicheza kufuata muziki kando ya baa (uk 6)
- Matumizi ya barua. Barua iliandikwa na Furaha katika uk 44. Katika barua hii Furaha ameweka orodha ya mambo yote yaliyomfanya akapata UKIMWI.
- Matumizi ya nafsi. Mwandishi kwa kiasi kikubwa ametumia nafsi ya kwanza umoja na wingi. Pamoja na hayo, matumizi ya nafsi ya pili na ya tatu yameonekana.
MANDHARI
Mwandishi ametumia mandhari ya vijiji vya Afrika ya Mashariki. Pia ametumia mandhari ya: mtaani, kanisani, barabarani, hospitali, makaburini, baa, nyumbani, vichochoroni, chumani na sebuleni.
WAHUSIKA
Furaha.
- Mhusika mkuu
- Binti mdogo wa miaka kati ya 13 na 19
- Ni malaya
- Ni mwathirika wa UKIMWI
- Ni mlevi
- Ni mkweli na muwazi
-
Mama Furaha
- Ni mama yake Furaha
- Ni mkweli na muwazi
- Ana upendo
- Ni jasiri
- Ni mpole na mchapakazi
Baba
- Ni baba yake Furaha
- Ni mkali
- Ana upendo
Mary
- Ni rafiki yake Furaha
- Ni malaya
- Ni mlevi
- Anapenda anasa
- Anatamaa
Bwana Ecko
- Ni mwanaume mtu mzima
- Ni malaya
- Ni mlevi
- Ni muathirika wa ugonjwa wa UKIMWI
- Ni laghai kwa mabinti wadogo
Juma
- Ni muathirika wa UKIMWI
- Ni laghai kwa mabinti wadogo
- Ni mlevi
- Ana tamaa
- Anapenda anasa
Padri James
- Ni mtumishi wa Mungu
- Si muadilifu
- Anauogopa ukweli na uwazi
- Ni dhaifu kwa wanawake
Wahusika wengine ni: Kitunda, Salim, Wanakijiji na Dada Mdogo
Matumizi ya lugha
- Tamathali za semi
Sitiari. Mfano, Furaha Waridi changa zuri.
Tafsida. Mfano, mayai yangu madogo.
Mubaalagha. Mfano, kuna majengo makubwa kiasi kwamba unaweza kuona mlima Kilimanjaro kwa juu!
Tashibiha. Mfano, Furaha ni kama punda wa kijiji
Mdokezo. Mfano, ndiyo padre ni
Nidaa. Mfano, Ooo!
Takriri. Mfano, sana, sana sana sana.
Tashtiti. Mfano, Mama Furaha: wewe na marafiki zako wa kiume?
Furaha: marafiki gani wa kiume
Onomatopea/ tanakali sauti. myauuuu!
Misemo.
Furaha anavuna mbegu ya kifo aliyopanda.
Kufaulu na kutofaulu kwa mwandishi
Kufaulu
Kimaudhui
i. Mwandishi amefaulu kuonesha mambo yasababishayo UKIMWI na njia za kuepuka.
Kifani
i. Mwandishi ametumia wahusika ambao wameendana na kile alichotaka kuifahamisha jamii.
Kutofaulu
i. Mwandishi ameegemea mno kijijini, utadhani ugonjwa wa UKIMWI, unawahusu wakazi wa vijijini pekee.
ii. Katika muundo mwandishi ametumia onyesho moja tu liligowanyika katika sehemu ishirini. Tamthiliya hii ilipaswa iwe na maonyesho mengi zaidi.

NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE
NGOSWE -PENZI KITOVU CHA UZEMBE
MTUNZI: EDWINI SEMZABA
MCHAPISHAJI:THE GENERAL BOOKSELLERS LTD
CHAPA YA 1-1988
UTANGULIZI
N goswe-penzi Kitvu cha Uzembe inaonyesha namna jamii inapaswa kushiriki mipango mbalimbali ikiwepo ya kisiasa kiuchumi na kiutamaduni.Mafanikio ya mipango hiyo inategemea na kujulikana kwa idadi ya watu utayari,uelewa wa watu hao kuhusu mipango husika
Tamthiliya hii inaonyesha kazi ya kuhesabu watu ilivyokwama kijijini kwa mzee mitomingi ngengemkeni kutokana na uzembe wa afisa wa kuhesabu sensa Ngoswe.
DHAMIRA
MAPENZI
Mwandishi Edwin semzaba ameonyesha jinsi mapenzi yalivyo kitovu cha uzembe,wahusika Ngoswe na Mazoea wametumiwa na mwandishi kufafanua dhamira hii
Ngoswe baada ya kufika kwa mzee Mitomingi anashindwa kuitawala nafsi yake mara anapomuona Mazoea,Ngoswe aliamua kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na Mazoea hali iliyomfanya ashindwe kuimudu kazi yake na mapenzi kwa wakati mmoja.
Ngoswe anamtorosha Mazoea kitendo hiki kinamuudhi balozi Mitomingi Ngengemkeni (baba mzazi wa mazoea)na kuamua kuchoma moto karatasi muhimu za serikali.Ngoswe anaonekani ni mzembe kwa kuwa alishindwa kutofautisha kazi na mapenzi kama msomi (afisa wa sensa )alitakiwa ajue umuhimu wa kazi iliyompeleka kijijini.
LEVI NA ADHARI ZAKE
Katika tamthiliya ya ngoswe penzi kitovu cha uzembe mwandishi anaonyesha namna ulevi ulivyoleta madhara,mfano kuchelewesha kazi.Wahusika Mitomingi na Ngoswe wanashindwa kukamilisha kazi kwa vile wahusika (wahesabiwa)wapo kwenye Pombe kama maneno haya yanavyothibitisha;
Mitomingi:Haya ni matatizo yote hii shauri ya pombe nadhani yupo kilabuni
Ngoswe :hawezi kwenda kuitwa?
Mitomongi:haitosaidia mkewe tu hana habari ya kuhesabiwa sembuse hao wengine kwa leo haitowezekana
Licha ya kuchelewesha kazi ulevi huaribu kazi.Mfano:ngoswe anaunguza karatasi za sensa baada ya kulewa pombe ya mnazi.
ELIMU
Elimu ni chombo cha ukombozi kama itatumiwa vizuri ipaswavyo,mwandishi wa tamthiliya hii amemuonyesha kijana Ngoswe (msanii)alivyoshindwa kutumia elimu yake hususani katika kujua namna ambavyo maisha ya mjini yanavyotofautiana na maisha ya kijijini,Ngoswe anajikuta akiharibu kazi yake kwa kukosa maarifa.
Mwandishi ameonyesha elimu katika familia ya mito mingi haikupewa thamani yoyote ile wananchi wengi hawakuwa na elimu kwa kisingizio cha shule kuwa mbali,ukosefu wa elimu ulichangia ukosekanaji wa huduma muhimu kama vile hospitali ,miundo mbinu na maji ili kupata maendeleo,suala la elimu lazima litiliwe maanani watu wakieleweshwa wataweza kujua wajibu wao :-
Mfano:kujali kazi na kuacha ulevi kutumia vema hospitali badala ya kutegemea mitishamba
UCHAWI NA USHIRIKINA
Mwandishi wa tamthiliya hii ameonyesha jinsi watu wengi ndani ya jamii walivyo na imani juu ya uchawi,wanajamii hawa wameweka vikwazo kuhusu sensa wakiamini kuwa mtu anayewahesabu wenzake ni mchawi
Mfano:mama anasema mchawi ndiyo huhesabu watoto wa wenzake ili awaroge sasa wewe ni mchawi? hata kama si mchawi siwezi kukubali unihesabu maana sijui nia yako kama ni mbaya au nzuri.Imani hizo ni za kishirikina zinachangia kukwama kwa zoezi la sensa pia maendeleo kwa ujumla kuwachini,watu wakiugua hawapelekwi hospitali badala yake wanapelekwa kwa mganga wa kienyeji wakidhani kuwa amerogwa.
5. NAFASI YA MWANAMKE
Katika tamthiliya hii mwanamke ametazamwa katika mitizamo tofauti kama ifuatavyo;
wanamke amechorwa kama chombo cha starehe ,mwandishi amemuonyesha mzee mitomingi kuwa na wake wengi (mitala)bila kuoyesha bayana kazi zao.
wanamke amechorwa kama mtu asiye na sauti
mfano:Mazoea na mama yake hawakushirikishwa katika mipango ya kutaka kuolewa mazoea kwa vile walionekana hawana mchango wowote katika maamuzi hayo
wanamke amechorwa kama mlezi,
katika tamthiliya hii inamchora mwanamke kama mtu mwenye majukumu ya malezi ya watoto,baada ya Mazoea kuwa na mahusiano na Ngoswe mzee Mitomingi anamlaumu mama yake Mazoea kuwa hakuona dalili ya mahusiano ya kimapenzi kwa kuwa ni jukumu la mama kumwangalia binti yake.
DOA NA MALEZI
Mwandishi wa tamthiliya hii ameonyesha suala la ndoa ni suala la hiyari na si kufuata matakwa ya wazazi,Mazoea alichaguliwa mchumba na wazazi wake (baba yake)hali iliyomfanya kutoroka na ngoswe
Hali kadhalika katika tamthiliya hii wanaume wengi wana mke zaidi ya mmoja hali hii inapelekea familia kuwa kubwa na kushindwa kuzitunza.
Mfano:Mzee Mitomingi ana wake wawili ambao ni mama Mazoea na mama Mainda,wazazi hawa wanatofautiana katika malezi hasa kwa Mazoea hali iliyopelekea kuwa na tabia mbaya.
Kwa upande mwingine ndoa zenye mke zaidi ya mmoja haziwi na upendo ndani ya familia hivyo kuwa kikwazo kwenye malezi.
6. UVIVU NA ATHARI ZAKE
Wanakijiji wa Ngengemkeni mitomingi wengi ni wavivu muda mwingi wanautumia kwenye ulevi na uvuvi,unawafanya wakose huduma muhimu kama shule,barabara na hospitali huduma hizi zingepatikana kama wananchi wenyewe wanajitolea.
Siku zote wavivu wanatafuta visingizio,vifo vingine vinatokea sababu ya uzembe na uvivu kisha sababu hutafutwa.
Mfano:wanawake wawili walidai mume wao amerogwa ili hali wenyewe hawakumpeleka hospitali
MIGOGORO
Ni hali ya kutoelewana baina ya pande mbili zenye mitazamo tofauti Katika tamthilia ya
Ngoswe penzi kitovu cha uzembe kuna migogoro mingi ambayo imeweza kujitokeza kama ilivyoonyeshwa na mwandishi
gogoro kati ya Ngoswe na wazazi wa Mazoea chanzo cha mgogoro huu umetokana na Ngoswe kumtorosha Mazoea,suluhisho wazazi kumfukuza Ngoswe na Mazoea kuchoma karatasi na kumwadhibu Mazoea
gogoro kati ya Mazoea na wazazi wake,chanzo cha mgogoro huu ni baada ya Mazoea kutoroka na Ngoswe ili hali Mazoea tayari ana mchumba wake,suluhisho ni mitomingi kumchapa mazoea na kuchoma karatasi za sensa.
gogoro kati ya Ngoswe na serikali,chanzo cha mgogoro huu ni Ngoswe kuharibu kazi ya sensa na hivyo kusababishia serikali ishindwe kupanga mipango ya maendeleo,suluhisho halijapatikana hadi mwisho.
UJUMBE
jambo zuri kuchanganya suala la kazi na starehe au mapenzi,wakati wa kazi uwe wa kazi na wakati wa starehe uwe wa starehe
avulana wanaovuruga wasichana siku moja watakamatwa na wasichana wenyewe wanapewa tahadhali wasiwe na maamuzi bila kufikilia.
imu ni kitu cha muhimu sana katika jamii na jamii isipokuwa na watu walioelimika hawawezi kuwa na maendeleo maana ili tuwe na maendeleo tunatakiwa tutupilie mbali ulevi na uvivu katika jamii yoyote
hawi na ushirikina ni kikwazo kikubwa katika maendeleo
FALSAFA
Mwandishi anaamini kuwa ni rahisi jamii kuingia kwenye matatizo kama itachanganya mambo mengi kwa wakati mmoja hivyo ikumbukwe kuwa kila jambo na wakati wake.
FANI
Vipengele vya fani katika kazi ya fasihi ni muundo ,mtindo,madhari ,wahusika na matumizi ya lugha
MUUNDO
Muundo uliotumika katika tamthiliya ni wa
muundo wa moja kwa moja ambapo kazi nzima ipo katika sehemu tano ambazo mwandishi amezipa majina ya kitwasira kulingana na ukubwa wa tatizo linalozungumziwa ,yaani ameonyesha kuingia kwa Ngoswe kijijini mazingira yanayoashiria hali ngumu ya maisha( kijito)
hemu ya pili inaonyesha kazi ya kuhesabu watu imeanza na watu hawana utayari na uelewa juu ya sensa ( vijito )
hemu ya tatu inaonyesha Ngoswe ameanza kujihusisha na mapenzi na ulevi,ambavyo ni viashiria vya kuharibu kazi yake ( mto)
hemu ya nne inaonyesha kazi aliyopewa Ngoswe tayari imekosa mwelekeo,Ngoswe amebobea kwenye mapenzi na ulevi, karatasi zinachomwa moto baada ya kumtorosha Mazoea ( jito)
hemu ya tano inaonyesha serikali ikimuhukumu Ngoswe juu ya takwimu zilizoungua moto na Ngoswe asingizia kuwa kijijini kuna shida ya kuhesabu kwani nyumba zimejitenga na watu wenyewe kutoelewa ( baharini )
MTINDO
Mtindo uliotumika ni wa kidayalojia ambapo wahusika wake wanazungumza kwa kujibizana
Pia kuna matumizi ya nafsi zote tatu na nafsi hizo zimetumika katika sehemu mbalimbali.Mfano sehemu ya tano kwa matumizi ya nafsi ya kwanza pale Ngoswe anapoulizwa na serikali kuhusu takwimu akajibu usemi sinao
MANDHARI
Kitabu hiki kimejengwa katika mandhari ya kijijini,hii inadhihirishwa na ukosefu wa huduma muhimu kama vile shule hospitali na miundo mbinu
Tabia za wahusika pia zinaonyesha mandhari ya kijijini mfano,ulevi wa pombe za mnazi,watu kutojali elimu,kungangania mila zilizopitwa na wakati
MATUMIZI YA LUGHA
Mwandishi ametumia lugha nyepesi na yenye kueleweka pia mwandishi ametumia tamathali za semi,misemo na mbinu nyingi za kisanaa.
Tamathali za semi
Hizi ni semi au kauli zitumiwazo na mwandishi katika kazi ya fasihi ili kuongeza ladha katika kazi husika
Tashibiha
Ni tamathali ilinganishayo vitu viwili au zaidi kwa kutumia viunganishi kama mithili ya ,kama,mfano wa
Mfano,Ngoswe anaposhangaa ardhi ya kijijini kwa balozi Mitomingi anasema
Udongo mwekundu kama ugoro wa sabiani
Tazama suruali yake kama kengele ya bomani
Nikitoka hapa najitupa kitandani kama gogo
Tafsida
Ni tamathali itumiwayo kupunguza ukali wa maneno
mfano Mainda anasema labda anajisaidia(Uk 21)
Takriri
ni tamathali inayorudiarudia neno ili kuweka mkazo juu ya kile kinachosemwa
Mfano; karibu,karibu(pale Ngoswe alipokuwa akikaribishwa)
Mdokezo
Ni tamathali ambayo hueleza jambo kwa kukatakata maelezo
Mfano Mazoea anasema sijui......sijui......siwezi namwogopa baba (Uk 22)
Tanakali za sauti
Ni tamathali inayoiga mlio wa vitu
mfano Ngoswe alishindwa kujizuia akacheka ha ha ha ha
Methali
Ngoswe anamwambia Mazoea
v Penye nia pana njia (uk 22)
Misemo
ebu keti tutupe mawe pangoni
peleka chakula ndio unafanya makambi
Taswira/Jazanda
Taswira mbalimbali zimetumiwa na mwandishi katika tamthiliya hii. Msanii ametumia taswira ya mtu kwa kuhusisha na matukio ya wahusika.Mwandishi analinganisha mwanzo wa mchezo ni kijito ni mto mdogo sana hivyo maelezo ya sehemu hii yanategemewa kuwa madogo sana
hemu inayofuata ya vijito,sehemu ya vijito inaonyesha kuwa masuala yanashughulikiwa na kujadiliwa hapa yanaongeza uzito ingawa sio mazito sana
hemu ya mto inaonyesha ukubwa wa shughuli ya Ngoswe yuko kazini (yuko mtoni)tayari yupo ndani ya jukwaa bila shaka maji ya mto ni mengi (matatizo mengi)na hivyo yeyote atakayeingia mtoni yampasa awe mwangalifu
hemu ya jito inaashiria kuna hatari, kuna matatizo mengi, katika jito kulivika si kazi rahisi hatimaye tunaonyeshwa Ngoswe amezama baharini ambapo kuzama kwa Ngoswe ni baada ya makaratasi kuchomwa moto.
WAHUSIKA
Wahusika ni watu walioshiriki katika mchezo au tamthiliya husika.
Mwandishi amegawa wahusika katika makundi mawili yaani mhusika mkuu na wahusika wasaidizi
MHUSIKA MKUU
NGOSWE
Ni msomi anayependa kazi ya kuhesabu watu lakini kutokana na tamaa ya mwili wake anaharibu kazi baada ya takwimu zote kuchomwa moto na Mitomingi kutokana na kitendo cha kujaribu kumtorosha mazoea .
WAHUSIKA WADOGO
Mazoea
sichana mwenye umri wa miaka 18-20
i mtoto wa balozi (Mitimingi)
awakilisha wanawake wasio na msimamo katika mapenzi
Ngengemkeni mitomingi
uyu ni balozi
ba yake Mazoea
achoma karatasi za takwimu kutokana na Ngoswe kutaka kumtorosha Mazoea
i mzee aliyeshikilia ukale na anapenda ndoa za mitara
JINA LA KITABU
Ngoswe penzi kitovu cha uzembe jina hilo la kitabu linasadifu yaliyomo ndani ya kitabu ,kwani msanii kwa kiasi kikubwa amejaribu kujadili na kuonyesha matatizo yanayoikumba jamii katika shughuli za kijamii,matatizo hayo ni kama uchawi ulevi uzembe na dhana nyingine potofu
KUFAULU NA KUTOFAULU KWA MWANDISHI
Mwandishi katika tamthiliya hii amefeli kwa kuwa ameonyesha matatizo yaliyomo katika jamii bila kuonyesha mbinu mbadala ya kuyatatua.

UHAKIKI WA FASIHI ANDISHI
JINA LA KITABU: NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE
MWANDISHI: EDWIN SEMZABA
Utangulizi
Afisa aliyetumwa kuhesabu watu-Ngoswe, anashindwa kuifanya kazi yake na kuanzisha ajenda nyingine ya mapenzi. Anapanga kutoroka na binti Mazoea aliyekwisha kuposwa tayari, Mazoea naye kusikia atakwenda kuishi mjini anakubaliana na mpango huo.
Wanapotoroka, Ngoswe anasahau mkoba wenye takwimu za watu waliokwisha kuhesabiwa, Mzee Ngengemkeni Mitomingi ambaye ndiye baba yake na Mazoea, anazichoma moto takwimu hizo na kumsababishia hasara kubwa Ngoswe.
Jina la Kitabu
Jina la kitabu Ngoswe penzi kitovu cha uzembe ni jina ambalo limesawiri vyema yaliyomo ndani ya kitabu hicho, kwani Ngoswe ndio jina la mhusika mkuu anayebeba dhamira kuu ya tamthiliya. Pia penzi limeonekana kuwa ni kitovu cha uzembe kwani ndio yaliyopelekea kuteketezwa kwa karatasi za takwimu za sensa. Hivyo jina la kitabu si tu kwamba limesawiri yaliyomo katika kitabu bali pia katika jamii.
Maudhui
Dhamira
1. Mapenzi
Mapenzi yametajwa kuharibu kazi katika tamthiliya hii. Ngoswe anampenda msichana Mazoea na kuamua kutoroka naye, baba yake Mazoea kwa hasira anachoma moto makaratasi ya sensa na kusababisha hasara kubwa.
2. Ulevi
Ulevi nao umeonekana kuwa chanzo cha uharibifu wa kazi. Wanakijiji wengo wanapofuatwa ili wahesabiwe, hawapo majumbani mwao, wapo katika pombe na hii inasabisha zoezi la kuhesabu watu liwe gumu.
Pia, Ngoswe na mwenyeji wake Ngengemkeni Mitomingi walikunywa pombe ya mnazi na kuharibu baadhi ya makaratasi ya sensa.
3. Suala la elimu
Jamii ya Mzee Mitomingi haikuzingatia elimu kwa watu wake. Watoto wengi hawakwenda shule kwa madai kuwa, shule zilijengwa mbali na makazi ya watu. Suala hili linadumaza na kukwamisha maendeleo ya muhimu kwa wanajamii.
4. Ndoa za mitara
Ngengemkeni ana wake wawili: Mama Mainda na Mama Mazoea. Kuoa kwake wake wawili, kunamfanya awe na familia kubwa ambayo huenda ndiyo sababu ya yeye kushindwa kutoa huduma stahiki hata kusababisha binti yake alaghaiwe kwa urahisi.
Pia, inatia shaka kama kweli Mitomingi aliwapenda wake zake wote kwa upendo wa kipimo sawa.
5. Imani za kishirikina
Wanakijiji wanaamini katika ushirikina na mambo yasiyofaa. Mama anakataa kuhesabiwa kwa madai kuwa, anayefanya hivyo ni mchawi na lengo lake ni kuwahesabu watu ili baadaye awaroge. Upuuzi huu unaonesha kazi ngumu ya kutoa elimu vijijini na wakati mwingine hata mjini ili kuleta ujenzi wa jamii mpya.
6. Nafasi ya mwanamke katika jamii
Tamthiliya ya Ngoswe inamchora mwanamke katika vipengele mbalimbali. Vipengele hivyo ni:
- Chombo cha Starehe:
Kijiji cha Ngengemkeni inaonekana kuwatumia wanawake katika starehe. Dhana hii inathibitishwa na tabia ya kuoa mitara kila mara; ili wanawake watumike kukidhi haja ya wanaume.
- Mama Mzazi na mlezi wa familia:
Wanaonekana wanajishughulisha na kazi za malezi baada ya kuzaa.
- Duni na asiye na mchango katika maisha:
Mwanamke anadharauliwa na wanaume na kumfananisha akili zake na mtoto. Mwanamke haelekei kuthaminiwa na kufikiriwa kuwa anaweza kuchangia jambo lolote la maana. Wakati Mazoea anatoroshwa na Ngoswe. Mitomingi anauliza:
MITOMINGI:
(...) Hivyo na nyie hamkuona dalili zozote juu ya watu hawa wawili.
MAMAMAZOEA: Zilikuwepo.
MITOMINGI: Kumbe mliziona na mkanyamaza tu!
MAMAINDA: Sasa Baba mazoea tungefanya nini?
MITOMINGl: Mngefanya nini? Nyie wanawake akili zenu wote sawa. Si Mazoea, si mama yake. (...) (uk. 26)
Kauli hii inaonyesha kuwa Mitomingi hawezi kumthamini mke wake kwa sababu hana akili za kikubwa - ni kama za mtoto wake Mazoea! Tabia ya Mitomingi ni ya wanaume wengi - jambo ambalo lazima lipigwe vita.
- Mwenye tamaa na maisha mazuri
Mazoea anatamani kuishi maisha mazuri ya mjini ndiyo sababu ya yeye kukubali kutoroshwa na Ngoswe.
Ujumbe
1. Tusiendekeze mapenzi kiasi cha kuharibu kazi
Ngoswe anaharibu kazi kwa sababu ya kuendekeza mapenzi.
2. Ulevi ni chanzo cha uharibifu wa kazi
Ngoswe na Mzee Mitomingi ni walevi, kazi zao zinasuasua. Pia, wanakijiji nao hawapatikani majumbani mwao kwa sababu muda mwingi wanautumia kuwa katika vilabu vya pombe.
3. Elimu itolewe maeneo yote, mjini na vijijini ili kufuta ujinga
Kijiji cha Mzee Mitomingi watu wake hawana elimu ya kutosha. Watoto wengi hawaendi shule kwa sababu shule ziko mbali na makazi yao.
4. Imani za kishirikina zinarudisha nyuma maendeleo ya jamii
Kuamini katika ushirikina kunasababisha zoezi la sensa liwe gumu hasa pale Mama anapokataa kuhesabiwa kwa madai kuwa, anayefanya hivyo ana mpango wa kuwaroga watu.
Migogoro
Migogoro ya wahusika
Ngoswe na Mitomingi
Mgogoro huu unasababishwa na Ngoswe kutoroka na Mazoea. Mitomingi anaamua kuyachana makaratasi ya sensa.
Mitomingi na wake zake
Mgogoro huu unasababishwa na kitendo cha kutoroshwa kwa Mazoea na Ngoswe. Ana hoji kwa nini wake zake hawakutoa taarifa mapema ikiwa dalili waliziona.
Mama na Ngoswe
Mgogoro huu unasababishwa na Ngoswe kutaka kumhesabu Mama. Anakata kwa madai kuwa, anayefanya hivyo ni mchawi.
Kifaruhende na Mitomingi
Mitomingi anamlaumu Kifaruhende kwa kitendo chake cha kutokuwa nyumbani wakati alipewa taarifa kuwa, zoezi la uhesabuji watu linaendelea.
Migogoro ya nafsi
Mgogoro huu unampata Mazoea pale anapotongozwa na Ngoswe. Anawaza akubali au akatae hasa ukizingatia tayari alikuwa amechumbiwa na mwanamume mwingine. Mazoea, anaamua kukubali kuwa na Ngoswe na kuongozana naye mpaka mjini.
Pia, mgogoro wa nafsi unampata Ngoswe baada ya makaratasi ya sensa kuchomwa moto. Anawaza ataieleza nini serikali iliyomtuma. Vipi hatma ya ya kazi yake ukweli ukijulikana?
Falsafa
Mwandishi anaamini kuwa, mapenzi yakizidi huleta hasara.
Msimamo
Mwandishi ana msimamo wa kimapinduzi kwa sababu anaamini kuwa, mapenzi yakizidi sana ni hasara. Katika matatizo makubwa yasababishwa na mikasa ya mapenzi, mwandishi ana shauri watu wapende kwa kiasi na kamwe wasichanganye mapenzi na kazi.
Fani
Mtindo
Dayolojia
Mtindo huu wa majibizano umetumiwa kwa kiasi kikubwa. Wahusika wengi wanajibizana.
Monolojia
Kwa kiasi kidogo mtindo huu wa masimulizi umetumika ili kufafanua zaidi vitendo vinavyofanywa na wahusika.
Matumizi ya nafsi
Nafsi zote tatu zimetumika. Hata hivyo, matumizi ya nafsi ya kwanza yametawala.
Muundo
Tamthiliya hii imetumia muundo wa moja kwa moja. Inaanza kwa kumuonesha Ngoswe akiwa katika kijiji cha Mzee Mitomingi, akianza kazi zake, akitoroka na Mazoea na mwisho karatasi za sensa zikichomwa moto.
Pia, matukio haya yamepangwa katika maonyesho matano.
Wahusika
Ngoswe
- Kijana anayeaminiwa na serikali kwenda kuhesabu watu
- Ni mlevi
- Anaendekeza mapenzi na kujikuta akiharibu kazi
Mazoea
- Mtoto wa kike wa Mzee Mitomingi
- Hana elimu
- Ana tamaa. Pamoja na kuwa alikuwa tayari kaposwa, alimua kuwa na Ngoswe.
Ngengemkeni Mitomingi
- Ni balozi katika kijiji chake
- Ana wake wawili
- Baba yake Mazoea
- Ana hasira sana. Hili linathibitika pale anapochoma moto makaratasi ya sensa.
Mzee Jimbi
- Hana elimu
- Ni mlevi
- Hajui umri wake
Mama Inda na Mama Mazoea
- Wake zake Mitomingi
- Hawana nafasi ya kufanya maamuzi
Mandhari
Mandhari ya tamthiliya hii imechorwa katika mazingira ya kijijini. Maeneo mbalimbali yanaonekana kama: shambani, katika vilabu vya pombe, chumbani, kisimani, nyumbani n.k.
Matumizi ya lugha
Matumizi ya semi (Nahau, misemo na methali)
Methali
Uk.22 Penye nia pana njia.
Uk.27 Waona vyaelea vyaundwa.
Misemo
Uk.14 Akuwaniae uovu haji kweupe
Nahau
Uk.11 hebu keti tutupe mawe pangoni tule chakula
Uk.7 mbongo zimelala- ana maarifa
Uk.14 pombe na yeye ni pete na chanda- anapenda pombe sana.
Matumizi ya tamathali za semi
Tafsida
Uk.21 Wala hajarudi, kama ingekuwa ni kujisaidia si angekuwa amekwishamaliza?
Tashibiha
Uk.1 vumbi jekundu kama ugoro wa subiana
Uk.8 sarawili yake miguuni kama kengele ya bomani
Mubaalagha
Mama mazoea : Kujibu swali ndio ukachukua mwaka mzima!
Mbinu nyingine za kisanaa
Mdokezo
Uk.22 Mazoea : sijui siwezi namuogopa baba
Uk.16 Ngoswe : huyo mtoto wenu wa kwanza anaishi hapa au..
Takriri
Uk.9 Mama Masikio! We Mama Masikio!
Uk.13. Hodi! Hodi!
Uk.2 karibu karibu
Tashtiti
Uk.5 Ngoswe: hivyo waitwa nani?
Mazoea: mie?
Hapa wahusika waliuliza maswali ambayo majibu yake waliyaelewa ila kutokana na kutaka kudhihirisha hasira, msisitizo nk. Ndio maana wametumia tashtiti.
Ujenzi wa taswira
Mwandishi anaeleza matukio na kuwafanya watu wawe kama wanaona kitu katika luninga, usomapo kazi hii, utakuwa kama unaona vitu fulani ubongoni. Tazama mfano huu,
Mazoea aingia ndani huku macho ya Ngoswe yakiwa mgongoni kwake. Atikisa kichwa, na mara hiyohiyo Mitomingi na wazee wawili wanaingia.
Kufaulu kwa Mwandishi
Mwandishi amefaulu kuonyesha athari za mapenzi endapo yataendekezwa kupita kiasi.
Kutofaulu kwa Mwandishi
Mwandishi hajaonyesha faida za mapenzi. Yeye kaegemea katika hasara pekee, jambo hili si kweli kwani kwa kiasi fulani mapenzi yana faida

Subscribe to:
Posts (Atom)